MREMBO anayekimbiza na ngoma ya
Ulithemba, Esterlina Sanga ‘Linah’, juzikati alifunguka kwamba, wivu wa
mchumba wake Nangari Kombo ‘Nanga’, nusura umkoseshe mamilioni ya fedha
alizopewa kwenye udhamini na Kampuni ya Serengeti.
Msanii wa muziki wa bongo fleva, Esterlina Sanga maarufu kama ‘Linah’.
Akiteta na paparazi wetu ndani ya Ukumbi wa Escape One, Mikocheni
jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alisema katika maisha yake ya
kimapenzi amejifunza jambo muhimu sana la kupunguza wivu kwani ukizidi
sana unaweza kumsababishia mtu kukosa vitu vya maana kwenye maisha.
“Nimeamini wivu ni adui mkubwa wa maendeleo kwenye maisha maana kama
usipoweza kuuzuia unaweza kujikuta ukishindwa kutimiza ndoto zako kama
ilivyotaka kunitokea kwani kila mara nilipokuwa nikiongea na bosi wa
Serengeti mchumba wangu alikuwa akinikoromea hivyo kama ningemsikiliza
nisingepata hili dili,” alisema Linah.
إرسال تعليق