Kwenye zile info zilizosikika leo kwenye 255, msanii Linex amezungumzia wimbo wake mpya wa salima aliomshirikisha Diamond Platimuz
aliouachia leo, amesema leo anasambaza wimbo huo kwenye vituo
mbalimbali vya Radio na Television na yuko kwenye mikakati ya kuipeleka
kwenye vituo vikubwa vya Television nje ya nchi, ambapo Audio ya wimbo
huo imefanywa na producer Tuddy Thomas huku video ikifanywa na director mkali Bongo Adam Juma.
Msanii Lina
amezungumzia tukio alilolifanya leo la kusaini dili la kuwa Balozi wa
kinywaji kipya cha Jebel dili alilopata kutokana na ushawishi mkubwa
alionao kwa watu ambalo atafanya kwa mwaka mzima, ukiwa ni mkataba wake
wa tatu kwani alishaingia mikataba mingine miwili ya kuwa Balozi wa
vitu tofauti na inamsaidi kupata fedha za kujiendeleza kwenye mziki.
Story ya mwisho kwenye 255 inahusu video aliyoposta muigizaji Aunty Ezekiel kwenye ukurasa wake wa Istagram
jana usiku ,ikimuonyesha akiwa Hospitali na watu wakaanza kumpongeza
kwa kujifungua, baada ya siku yake kutokuwa hewani 255 iliamua kumtafuta
Mose Iyobo anaesemekana kuwa baba wa mtoto huyo, ambae amesema kuwa alikuwa anashoot video ya movie mpya aliyocheza na msanii Dude.
Ili kuweza kusikiliza story zote za 255 bonyeza play hapa chini…

Post a Comment