Twitter imeamua kudhibiti matumizi mabaya ya Mtandao
Mtandao wa Twitter umebadili sheria zake katika kuzuia watumiaji wake kuchapisha Picha na video chafu.
Sheria
ya mtandao huu wa kijamii inasema ''Marufuku kuchapisha picha au video
chafu zilizopigwa au kurekodiwa kisha kusambazwa bila ridhaa ya muhusika
aliye kwenye video na picha hizo''
Mwezi uliopita vitendo hivi vilitambulika kuwa makosa ya jinai uingereza na Wales.
Msemaji wa Kampuni ya Twitter amesema watumiaji watakaobainika kukiuka masharti mapya ''Anuani zao zitafungiwa''
Watumiaji
wanaopeleka malalamishi Twitter kuhusu picha na Video zilizochapishwa
watatakiwa kujitambulisha na kuithibitishia Kampuni kuwa hawakuwahi
kutoa idhini ili kuchapisha picha au video mtandaoni na kuonekana kwa
hadhira.
Yeyote atakayebainika kuchapisha picha hizo kinyuma na
utaratibu wa sheria hii mpya atatakiwa kufuta kwanza kabla ya kurejeshwa
tena mtandaoni.
Nchini Uingereza na Wales imeweka sheria ambayo mtuhumiwa atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka miwili gerezani.
Sheria hiyo inagusa picha zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii na Ujumbe mfupi.
Majimbo kadhaa ya Marekani wameweka Sheria ya kupambana na vitendo hivi hasa California,Texas na Utah.
Mabadiliko
haya ya twitter yamekuja baada ya Kampuni hiyo kukosolewa kuwa imekuwa
haifanyi jitihada madhubuti dhidi ya matumizi mabaya ya mtandao
unaofanywa na watumiaji wake(BBC)

Post a Comment