Linex
akimshirikisha Diamond Platnumz katika wimbo wake mpya salima ambao leo
hii ameuachia katika media mbalimbali. Video na audio ametoa kwa
pamoja, linex anaonekana kutulia sana katika wimbo huu, kama kawaida
yake ametumia lugha 3 ndani ya wimbo, amepanga mashairi mazito yenye
hisia hakika wimbo upo sawa, na utunzi na ghani za mashairi
yamepangiliwa katika ubora wa aina yake, lugha imetumika kihufasaha
wimbo ni mzuri kwa ujumla ukiusikiliza hasa pale Diamond Platnumz
alipofuata nyayo za uimbaji wa linex……….. ametumbukiza maneno ya kilugha
kama afanyavyo linex katika kila nyimbo zake anazoimba hakika Diamond
ameutendea haki wimbo huu, wimbo unagusa nyoyo za watu…..wimbo unagusa
hisia……na tena wimbo unaweza ukakutoa machozi..! welldone
Linex….welldone Diamond….welldone team nzima na management inayomsimamia
Linex kufanikisha kuutoa wimbo huu
Video – linex ft diamond – Salima
Video
ya wimbo huu ni ya kuvutia sana, pongezi kubwa sana kwa aliyeandaa
siclipt za video hii, video inatazamika kwa kila rika, video
hii……natumaini inaweza kutumika na baraza la mitihani ya taifa ya kidato
cha nne ama cha sita kuwatengenezea maswali kwa somo la
Kiswahili….sitashangaa nikiona wimbo wa salima wa linex ikiwa mojawapo
ya maswali ya mtihani wa ngazi ya taifa, its fantastic video!……natumaini
video hii itafanya vizuri zaidi hasa nje ya nchi yetu kwani ni video
inayoonyesha uhalisia wa kitanzania kabisa…………… hakika linex pamoja na
Diamond Platnumz wamefanya kazi kubwa na wavutia kwenye hii video,
Pongezi za ziada ziende kwa AJ ( huyu ni Adam Juma) amefanya kazi ya
ziada kwa kushuti kwa ustadi wa hali ya juu video hii…..kwakweli naweza
kusema hii ndio video bora kwangu kwa mwaka huu 2015 ingawa mwaka
haujaisha nimependa sana rangi nan a visa vilivyomo kwenye wimbo huu
video ina mafunzo nani nzuri sana!!!…..big up Adam Juma.
إرسال تعليق