STAA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekiri kuwa ubize wake
katika masomo umemzuia kwa kiasi kikubwa kupata muda wa kufikiria mambo
ya kijinga na hata kujirusha.
Staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akichonga na paparazi wetu juzikati, Lulu alisema mtu akisimamia
kwenye masomo hawezi kuwa na mawazo mabovu kama ya kwenda kujirusha au
kupata kilevi badala yake unajikuta ukifikiria masomo na mitihani tu.
“Jamani kama mimi sasa hivi sina hata ninachokiwaza zaidi ya masomo
yangu na mitihani ninayokutana nayo yaani hata muda wa kusema utaenda
Club, hakuna nafasi kabisa katika kichwa, hivyo nimeamini kuwa ukiwa
bize na masomo akili za ajabu hazipo kabisa,” alisema Lulu.

إرسال تعليق