MWANAMKE AMKATA MAMA MJAMZITO TUMBONI, AMWIBIA MTOTO

Dynel Lane anayetuhumiwa kwa kumkata mama mjamzito na kumwibia mtoto wake.
MWANAMKE mmoja aitwaye Dynel Lane (34), anashikiliwa na Jeshi la Polisi huko nchini Marekani kwa kosa la kumkata tumbo mama mjamzito na kumwibia mtoto wake.
Maofisa wa polisi wakiwa maeneo ya nyumba ya mtuhumiwa huko Longmont, Colorado nchini Marekani.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumatano iliyopita huko Longmont, Colorado nchini Marekani baada ya mjamzito huyo mwenye miaka 26 kwenda kwa mtuhumiwa kununua nguo za watoto.
Mama mjamzito alikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa kununua nguo za watoto baada ya kuona tangazo lililotolewa na Lane.
Kwa mujibu wa maofisa wa polisi, mama huyo mjamzito alipiga simu ya polisi '911' na kuongea kwa tabu kuwa: "Amenikata tumboni... Nina ujauzito....Ninatokwa na damu nyingi".
Hospitali ya Longmont United ambapo mama aliyekatwa tumbo lake alifanyiwa upasuaji na hali yake inazidi kuimarika.
Mama huyo mjamzito alikuwa na mimba ya miezi saba na polisi walipofika eneo la tukio walistaajabu kumkuta mama huyo akiwa amepigwa na kukatwa tumbo lake na mtuhumiwa huyo aliyetumia glasi iliyovunjika pamoja na kisu kutoa kichanga tumboni mwa mjamzito huyo.
Kutokana na taarifa ya mahakama, mtuhumiwa huyo alikuwa amewaambia ndugu na jamaa zake kuwa alikuwa na mimba na inawezekana alitaka kuwapelekea mtoto huyo ili awaonyeshe kuwa kajifungua.
Ofisa wa polisi akichukua maelezo ya mkazi wa eneo lilipotokea tukio hilo la kusikitisha.
Baada ya kufanya tukio hilo la kinyama, Lane alikwenda na mtoto huyo ambaye baadaye alifariki katika hospitali moja ambapo aliwaambia madaktari kuwa mimba yake imeharibika.
Mama huyo anayedaiwa kuwa na watoto wawili wa kike alikamatwa na polisi akiwa hospitalini hapo ambapo ameshitakiwa kwa makosa ya kutaka kuua, kushambulia, udhalilishaji wa mtoto na kusababisha kifo

Post a Comment

Previous Post Next Post