Dynel Lane anayetuhumiwa kwa kumkata mama mjamzito na kumwibia mtoto wake.
MWANAMKE mmoja aitwaye Dynel Lane (34), anashikiliwa na Jeshi la
Polisi huko nchini Marekani kwa kosa la kumkata tumbo mama mjamzito na
kumwibia mtoto wake.
Maofisa wa polisi wakiwa maeneo ya nyumba ya mtuhumiwa huko Longmont, Colorado nchini Marekani.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumatano iliyopita huko Longmont,
Colorado nchini Marekani baada ya mjamzito huyo mwenye miaka 26 kwenda
kwa mtuhumiwa kununua nguo za watoto.
Mama mjamzito alikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa kununua nguo za watoto baada ya kuona tangazo lililotolewa na Lane.
Kwa mujibu wa maofisa wa polisi, mama huyo mjamzito alipiga simu ya
polisi '911' na kuongea kwa tabu kuwa: "Amenikata tumboni... Nina
ujauzito....Ninatokwa na damu nyingi".
Hospitali ya Longmont United ambapo mama aliyekatwa tumbo lake alifanyiwa upasuaji na hali yake inazidi kuimarika.
Mama huyo mjamzito alikuwa na mimba ya miezi saba na polisi
walipofika eneo la tukio walistaajabu kumkuta mama huyo akiwa amepigwa
na kukatwa tumbo lake na mtuhumiwa huyo aliyetumia glasi iliyovunjika
pamoja na kisu kutoa kichanga tumboni mwa mjamzito huyo.
Kutokana na taarifa ya mahakama, mtuhumiwa huyo alikuwa amewaambia
ndugu na jamaa zake kuwa alikuwa na mimba na inawezekana alitaka
kuwapelekea mtoto huyo ili awaonyeshe kuwa kajifungua.
Ofisa wa polisi akichukua maelezo ya mkazi wa eneo lilipotokea tukio hilo la kusikitisha.
Baada ya kufanya tukio hilo la kinyama, Lane alikwenda na mtoto huyo
ambaye baadaye alifariki katika hospitali moja ambapo aliwaambia
madaktari kuwa mimba yake imeharibika.
Mama huyo anayedaiwa kuwa na watoto wawili wa kike alikamatwa na
polisi akiwa hospitalini hapo ambapo ameshitakiwa kwa makosa ya kutaka
kuua, kushambulia, udhalilishaji wa mtoto na kusababisha kifo
إرسال تعليق