MWANAMKE mmoja mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, Violet
Manyondo (40) anadaiwa kumtesa na kumfanyia vitendo vya kikatili mtoto
wake wa kumzaa, anayejulikana kwa jina la David (14).David ambaye ni
mwanafunzi wa darasa la tano katika shule moja ya msingi iliyopo
Mzambarauni, Dar kwa sasa haendi shule kutokana na majereha aliyonayo
kiasi cha kuwaliza majirani.
Mtoto David akiwa na majeraha mwilini aliyosababishiwa na mama yake mzazi.
Akizungumza na Amani, mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina
lake, alisema ni mara yake ya kwanza kushuhudia mama akimtesa mtoto
wake wa kumzaa kama anavyofanya mama huyo.“Tunaomba vyombo vya haki za
binadamu hata Jeshi la Polisi kushughulikia tukio hili haraka
iwezekanavyo vinginevyo mtoto huyo ataathirika kisaikolojia, halafu cha
kushangaza, ana watoto watatu, lakini ni huyu tu ndiye anayekutana na
kipigo,” alisema jirani huyo.
Alisema katika kumsaidia kijana huyo, wamewahi kwenda kituo cha
polisi Gongo la Mboto, lakini polisi jamii walipokwenda nyumbani hapo,
waliambulia matusi.Mtoto David aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli mama
yake anamtesa kwa muda mrefu na kwamba hivi karibuni alikwenda
kumshtaki katika kanisa lao liitwalo Universal Ufalme wa Mungu,
Mzambarauni, Ilala, Dar na alipotakiwa kumwita mama yake alikataa
kwenda.
David akiwa nyumbani kwao.
“Baada ya mama kupata wito ule hata kanisani ameacha kwenda kwa
kuhofia kikao na ushauri wa viongozi wa kanisa. Sina cha kufanya wala
pa kwenda, namuomba Mungu anisaidie nimalize shule,” alisema kijana
huyo.
Kuhusu sababu za kuteswa, alisema hafahamu chochote, ingawa alihisi huenda ni kwa sababu ya baba yake kutopeleka hela ya matumizi nyumbani, kitu ambacho hata hivyo haifahamu kwani hamfahamu mzazi wake, zaidi ya kusikia kuwa ni dereva wa daladala.

Katika hali ya kushangaza, mama huyo alipotafutwa na gazeti hili, alijibu kijeuri;
“Yule ni mwanangu, naweza kumfanya lolote lile. Mimi ni mzazi wake, natakiwa kumrekebisha kwa njia yoyote.” Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Gongo la Mboto umesema unashukuru kwa kupata taarifa hizo, kwani watahakikisha wanafuatilia jambo hilo na kulipatia ufumbuzi.

Kamanda Msangi: “Ni kweli tukio hilo limetokea na inadaiwa kuwa
chanzo cha kifo cha mtu huyo ni kipigo kilichotokana na imani za
kishirikina.”
إرسال تعليق