TUME
ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imesisitiza kwamba tarehe ya kufanyika kwa
kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa ipo pale pale na hakuna
mabadiliko yoyote kama inavyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima
Kombwey alisema kwa mara kadhaa baadhi ya vyombo vya habari vimenukuliwa
vikiandika habari kuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Damian Lubuva
amesema kura ya maoni kuhusu katiba haitafanyika Aprili 30 kama
ilivyotangazwa awali.
Alisema
hakuna mabadiliko yoyote na endapo kutakuwa na mabadiliko ya tarehe ya
upigaji kura ya maoni kuhusu katiba inayopendekezwa taarifa rasmi
itatolewa kwa umma.
“Kwa
sasa kipaumbele kwa Tume ni kuhakikisha kuwa uboreshaji wa daftari la
kudumu la wapiga kura linafanyika na kukamilika kwa ufanisi ili
kuhakikisha kila mtanzania aliyetimiza miaka 18 anaandikishwa kwenye
daftari,” alisema.
Aliongeza
kuwa endapo daftari la kudumu la wapiga kura litakuwa halijakamilika
hadi ifikapo Aprili 30 mwaka huu, tume itatoa taarifa rasmi ikiwa ni
pamoja na kuelezea mwelekeo wa utaratibu huo katika Mikoa mingine.

إرسال تعليق