BAADHI ya viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), juzi Jumamosi walijikuta wakitofautiana baada ya mshambuliaji wa
Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, kuifungia timu yake hiyo bao la ushindi
katika dakika za majeruhi ilipopambana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Bao hilo liliiwezesha Simba kubakiza pointi mbili tu ili kuifikia Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Katika hali ya kushangaza, baadhi ya wajumbe wa TFF, waliokuwa katika mkutano mkuu wa shirikisho hilo uliofanyika juzi Jumamosi na jana Jumapili, walipagawa kwa furaha baada ya kupata taarifa za bao hilo la Okwi huku wengine waliokuwa ni wa Yanga kuonekana wakiishiwa pozi.

Bila ya woga wowote, wajumbe wanazi wa Simba walianza kupongezana
huku wakipeana mikono na kukumbatiana na viongozi wa Simba, rais wa
klabu hiyo, Evans Aveva pamoja na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’
ambao pia walikuwa mjini hapa kwa ajili ya mkutano huo.
“Tulikuwa tunawapongeza viongozi hao kwa kupata matokeo mazuri ya
ushindi katika mechi zao tatu mfululizo tena dhidi ya timu kubwa.
“Lakini pia kitendo cha kumsajili Okwi kinaonekana kuwa kilikuwa na
maana kubwa kwao kwani faida yake imeanza kuonekana, hiyo ndiyo ilikuwa
sababu kubwa ya sisi kuwapongeza viongozi hao,” alisema Jackson Songora,
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA), huku akiungwa mkono
na wajumbe wengine ambao pia walionekana kufurahishwa na matokeo hayo.

إرسال تعليق