OMMY DIMPOZ: KUTULIPISHA KODI KWA SASA NI KUTUONEA

Mwimbaji wa bongo fleva Ommy Dimpoz amesema kwa sasa kuwalipisha wasanii kodi ya mapato ni kuwaonea kwa vile linatakiwa kwanza somo elekezi na mfumo mzuri wa kuhakikisha kazi za wasanii haziibiwi.

Akiongea na kipindi cha “Ubaoni” cha EFM Ijumaa jioni, msanii huyo ambaye ameachia wimbo wake mpya kabisa “Wanjera” akasema: “Kabla ya TRA kuanza kutulipisha kodi wahakikishe kwanza kazi zetu haziibiwi na  watupe somo la namna ya kulipa kodi kinyume na hapo watakuwa wanatuonea.
“Kulipa kodi sio tatizo lakini watutengenezee mfumo mzuri, kazi zetu zinaibiwa sana na tunapoteza pesa nyingi,” alifafanua Ommy Dimpoz wakati akijibu swali iwapo ni sahihi kwa wasanii kuanza kulipishwa kodi kupitia kazi zao.
Ommy Dimpoz aliulizwa swali hilo kufuatia habari zilizotawala wiki iliyopita kuwa msanii Diamond anatakiwa kuwasilisha hesabu zake mamlaka ya mapato (TRA) ili kujua kama kuna pato linatokiwa kulipwa

Post a Comment

Previous Post Next Post