Mwimbaji
wa bongo fleva Ommy Dimpoz amesema kwa sasa kuwalipisha wasanii kodi ya
mapato ni kuwaonea kwa vile linatakiwa kwanza somo elekezi na mfumo
mzuri wa kuhakikisha kazi za wasanii haziibiwi.
Akiongea
na kipindi cha “Ubaoni” cha EFM Ijumaa jioni, msanii huyo ambaye
ameachia wimbo wake mpya kabisa “Wanjera” akasema: “Kabla ya TRA kuanza
kutulipisha kodi wahakikishe kwanza kazi zetu haziibiwi na watupe somo la namna ya kulipa kodi kinyume na hapo watakuwa wanatuonea.
“Kulipa
kodi sio tatizo lakini watutengenezee mfumo mzuri, kazi zetu zinaibiwa
sana na tunapoteza pesa nyingi,” alifafanua Ommy Dimpoz wakati akijibu
swali iwapo ni sahihi kwa wasanii kuanza kulipishwa kodi kupitia kazi
zao.
Ommy
Dimpoz aliulizwa swali hilo kufuatia habari zilizotawala wiki iliyopita
kuwa msanii Diamond anatakiwa kuwasilisha hesabu zake mamlaka ya mapato
(TRA) ili kujua kama kuna pato linatokiwa kulipwa

إرسال تعليق