Jeshi
la Polisi mkoani Morogoro, linamshikilia mkazi wa Manispaa hiyo,
Josephat Asenga (47), mwenye taaluma ya uhasibu, kwa tuhuma za kujifanya
Padri.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema kuwa, Asenga
alikamatwa juzi saa 10:30 jioni, katika maeneo ya Modeco, Kata ya
Mazimbu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Maria.
Kwa
mujibu wa Kamanda Paulo, mtuhumiwa huyo alifika parokiani hapo Juni
mwaka jana akiwa amevaa mavazi ya Padri na kujitambulisha kwa Paroko wa
parokia hiyo, Malt Dyfrig Joseph, kuwa yeye ni Padri anaishi Jimbo la
New York Marekani.
Kwa
mujibu wa kamanda huyo, baada ya kujitambulisha kwa Paroko huyo na
kuonesha kitambulisho chake, alimuomba Paroko huyo kumpangia zamu ya
kuendesha Misa ya Jumapili iliyofuata na kukubaliwa na Paroko huyo bila
kukagua vizuri kitambulisho chake.
Alisema
mara baada ya misa hiyo, Paroko alipata taarifa kutoka kwa msamaria
mmoja wa Kituo cha Amani cha Chamwino mjini hapa, kuwa Padri huyo feki
anaishi na mwanamke katika maeneo ya Ujenzi kinyume na taratibu za
upadri.
Baada
ya kupata taarifa hizo, inadaiwa Paroko huyo aliwaomba waumini
wamshawishi Padri huyo feki, afike parokiani hapo na baada ya kufika,
alihojiwa na Paroko huyo na kudai kuwa alipata upadrisho katika Jimbo
Kuu Katoliki Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa kamanda huyo, baada ya Paroko huyo kupata maelezo hayo
alifanya mawasiliano na Katibu wa Jimbo hilo la Dar es Salaam na
kujibiwa kuwa hakuna jina la Padri huyo.
Juzi
Alhamisi majira ya saa 10:30, Padri huyo feki alimpigia simu Paroko
huyo na kumuomba ampange kuendesha Misa Takatifu ya Jumapili parokiani
hapo, na kukubaliwa na paroko huyo na kumtaka afike kanisani.
Baada ya kufika, taratibu za kujulisha Polisi zilifanywa na askari walipofika kanisani hapo, walimkamata mtuhumiwa huyo.
Kwa
mujibu wa Kamanda huyo, baada ya kufanya mahojiano na mtuhumiwa,
alikiri kuwa yeye sio Padri na walipokwenda nyumbani kwake kwa ajili
ya kufanya upekuzi, walimkuta akiwa na majoho saba ya upadri.
Mtuhumiwa huyo ameendelea kushikiliwa Polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika
إرسال تعليق