Mvua
inayoendelea kunyesha jijini Dar, tayari imeanza kusababisha kero kwa
wakazi wa jiji hilo kufuatia mitaro ya maji machafu kufurika na
kuwafanya watu washindwe kutumia vizuri barabara.
Miongoni
mwa maeneo yaliyoathiriwa na mvua hiyo ni pamoja na Sinza, Afrika-Sana
na Bamaga-Mwenge ambapo mwanahabari wetu alishuhudia wananchi wakipata
usumbufu wa kuvuka barabara zilizojaa maji hali ambayo imesababisha
washindwe kufika katika shughuli zao kwa wakati.
إرسال تعليق