Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la
Mwanga na Waziri wa Maji Mh. Prof. Jumanne Maghembe mara baada ya
kuwasili katika kata ya Kileo jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro wakati
alipoanza ziara ya kikazi ya jimboni humo akikagua na kuhimiza ilani ya
uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali, Katika ziara
hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Taifa CCM.
Akizungumzia
tatizo la maji nchini kwa ujumla Prof. Maghembe amesema serikali iko
katika utekelezaji wa miradi ya maji awamu ya pili ambapo serikali
inatekeleza miradi ya maji katika miji mikuu mbalimbali hapa nchini,
ambapo ifikapo mwaka 2025 upatikanaji wa maji katika miji mbalimbali
kufikia asilimia 75% wakati katika jiji la Dar es salaam upatikanaji wa
maji utafikia asilimia 95, hata hivyo Prof. Maghembe amongeza kwamba
miradi hiyo inatekelezwa kwa gharama kubwa na serikali ina nia ya dhati
ya kumaliza tatizo hilo nchini kwa kiwango kikubwa. (PICHA NA KIKOSIKAZI
CHA FULLSHANGWE-MWANGA KILIMANJARO).
Mbunge
wa jimbo la Mwanga na Waziri wa Maji Mh. Prof. Jumanne Maghembe
akizungumza na wananchi katika kata ya Kileo ambapo alikagua ujenzi wa
nyumba za walimu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya sekondari ya Kileo wilayani Mwanga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Waziri Prof.
Jumanne Maghembe wakikagua skimu ya umwagiliaji kijiji cha Kivulini
wilayani Mwanga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Waziri Prof. Jumanne Maghembe
wakishiriki ujenzi wa mifereji ya skimu ya umwagiliaji kijiji cha
Kivulini wilayani Mwanga.
Wananchi
wa Kijiji cha Kivulini wakitafakari jinsi ya kukwamua pikipiki yao
ambayo ilikwama kwenye moja ya mifereji yenye tope katika skimu hiyo ya
umwagiliaji.
Nape Nnauye akijaribu kuendesha Skaveta mtambo wa kuvunia mpunga katika kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Nape Nnauye akishuka kwenye Skaveta mtambo wa kuvunia mpunga katika kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana wakati akiwasili katika kijiji cha Mangara Lembeni wilayani
Mwanga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Waziri Prof. Jumanne Maghembe
kushoto wakipiga makofi kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika ofisi
ya CCM tawi la Mangara Lembeni wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Waziri
Prof. Jumanne Maghembe akicheza ngoma ya asili ya wapare huku Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma hiyo wakati
alipowasili katika moja na vijiji alivyotembelea na kuzungumza na
wananchi wilayani Mwanga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Waziri Prof. Jumanne Maghembe
wakishiriki ujenzi wa jengo la KKKT Mwaniko wilayani Mwanga
Waziri
wa maji na Mbunge wa jimbo la Mwanga Prof. Jumanne Maghembe akizungumza
na wananchi katika kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo.
Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika
mkutano huo uliofanyika kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga mkoani
Kilimanjaro.
Post a Comment