Rais Kikwete Atuma Salamu za Rambirambi Kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kufuatia Ajali Mbaya ya Basi Iliyoua Watu 42 Mafinga Leo

Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea  Mafinga katika mkoa wa Iringa eneo lijulikanalo kwa jina la Changarawe, ambayo imepoteza uhai wa watu zaidi ya 40 waliokuwa wakisafiri kwa basi hilo na wengine kadhaa kujeruhiwa.
 
Katika salamu zake hizo, rais Kikwete amewahakikishia wafiwa wote kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba wa ndugu na jamaa zao na kuwaombea kwa mwenyezi mungu, mwingi wa rehema watu wote waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo wapone haraka, ili waweze kuungana tena na ndugu na jamaa zao.

Post a Comment

Previous Post Next Post