MSANII
wa muziki wa Bongo Fleva, Cyrill Kamikaze ‘Cyrill’ na Mbongo Muvi
Sabrina Omary ‘Sabby’ hivi karibuni walinaswa katika ufukwe wa Hoteli ya
Golden Tulip, Masaki jijini Dar wakiwa kimahaba na hivyo kuzidisha
tetesi kuwa wanatoka kimapenzi.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Cyrill Kamikaze ‘Cyrill’ na Mbongo Muvi Sabrina Omary ‘Sabby’ wakipozi kimahaba.
Chanzo chetu makini kilisema wawili hao walionekana hotelini hapo
wakiwa eneo la kuogelea na walipomaliza walihamia katika viti ambako
sasa walikumbatiana kimahaba kana kwamba hakuna mtu anayewaona.
Kwa nyakati tofauti walipoulizwa kuhusu tetesi za kuwa wapenzi na
ushahidi wa picha, kila mmoja alikana, wakidai zitakuwa ni picha za
kutengenezwa kwa sababu mchezo huo umekuwa maarufu siku hizi huku Sabby
akisisitiza kuwa angefika ofisini ili kujiridhisha na picha hizo ndipo
aweze kuzungumza, kitu ambacho hakukifanya.
إرسال تعليق