Siri imefichuka! Bwa’mdogo a.k.a Serengeti Boy kutoka Kundi la Makomando, Fredy Felix amesimulia namna alivyofaidi penzi la staa wa Bongo Movies, Jacqueline Walper Massawe ‘Wolper’.
Fredy Felix kutoka Makomando.
Akizungumza na GlobalTV Online kwenye mahojiano maalum juzikati, dogo
huyo alisema kuwa katika maisha yake ya kimapenzi hakuna mwanamke
ambaye aliwahi kutoka naye na kujiachia kwa furaha kama ilivyo kwa
Wolper.
“Kiukweli msichana pekee ambaye nimewahi kuwa naye katika mapenzi na kumpenda kwa dhati ni Wolper pekee.“Mara yangu ya kwanza kukutana naye ilikuwa kama ‘sapraiz’ vile (habari zinasema kwamba walikutana maeneo ya Kinondoni), alipoingia kwangu nashukuru naye alinipenda na kunifanyia kila nilichohitaji.

Staa wa Bongo Movies, Jacqueline Walper Massawe ‘Wolper.
“Nampenda sana Wolper na kila siku nimekuwa nikiahidi kwamba huyo
ndiye mwanamke pekee ambaye nitakuja kuishi naye hata kama ni uzeeni
maana ninampenda kutoka moyoni.“Sidhani kama moyo wangu utampenda
mwanamke mwingine kama nilivyompenda Wolper. Kiukweli niliinjoi sana
penzi lake,” alisema Fredy huku akijutia kumwagana naye bila sababu ya
msingi.
Alipotafutwa Wolper ili kupata undani wa ishu hiyo simu yake ilipokelewa na aliposomewa mashtaka yake alikaa kimya bila kujibu chochote. Hata hivyo jitihada za kumtafuta zinaendelea
Alipotafutwa Wolper ili kupata undani wa ishu hiyo simu yake ilipokelewa na aliposomewa mashtaka yake alikaa kimya bila kujibu chochote. Hata hivyo jitihada za kumtafuta zinaendelea

Post a Comment