Ndege za uokoaji zimerejelea shughuli
Polisi
nchini Ufaransa wameeleza kuwa hali mbaya ya hewa itakwamisha zoezi la
utafutaji miili ya watu wapatao mia moja na hamsini katika eneo la ajali
ya ndege na hivyo kuchukuwa siku kadhaa.
Hali ya anga imeathiri uokoaji
Siku ya jana ndege ya Ujerumani
ilianguka katika eneo la milima ya Alps huko Ufaransa na kuua watu wote
wapatao mia moja na hamsini waliokuwemo.
Waathirika wa ajali hiyo
wanatoka nchi mbali mbali ambapo arobaini na tano ni wahispania huku
zaidi ya sitini wakiwa ni wajerumani.
Kumi na sita, kati yao
walikuwa ni wanafunzi kutoka shule moja nchini Ujerumani ambao walikuwa
wakijerea kutoka katika ziara ya kutembelea Hispania.
Hali ya hewa katika Milima ya Alps nchini Ufaransa
Pierre-Henry Brandet msemaji wa
Wizara ya Mambo ya ndani amewaambia waandishi wa habari kwa zoezi la
kuuopoa na kutambua miiili ndio kinachoopewa kipau mbele.
"Kipaumbele
chetu ni kupata miili mingi kwa kadri tuwezevyo ili kuwafanya wataalam
wa utambuzi wa uhalifu waweze kuifanyia utambuzi.
Jamaa na marafiki ya walioathirika wakitoa rambirambi zao
Na sio miili pekee kitu
chochote ambacho kitatusaidia kuitambua miili kama vile mizigo ya abiria
ambayo atakuwa ameibeba itachukuliwa na itatuwezesha
kuupeleka mwili katika nchi aliyotoka lakini ni mapema kusema ni wakati gani."
Ndege za uokoaji
Naye Raisi wa Marekani Barack
Obama amesema kwamba taifa lake linaungana na mataifa ya Ujerumani na
Hispania katika kipindi hiki kigumu walichopoteza
wapendwa
wao."Nataka kusema kwamba mawazo na sala zetu tunazielekeza kwa marafiki
zetu walioko Ulaya ,na hasa kwa watu wa nchi za Ujerumani na
Hispania ,kufuatia ajali mbaya ya ndege iliyotokea nchini Ufaransa.
Utafutaji miili ukiendelea
Inaumiza kwa sababu ajali hiyo
imepoteza watoto wengi kwa wakati mmoja ,na walio wengi watoto
wachanga.nilimpigia simu kansela wa Ujerumani Angela
Merkel
natarajia kuongea na Raisi ama waziri mkuu wa Hispania Rajoy baadaye leo
kutoa salamu za rambi rambi kutoka kwa watu wa Marekani ,lakini pia
kutoa msaada wowote utakao hitajika wakati huu wa uchunguzi wa chanzo cha ajali iliyosababisha janga kubwa.."(BBC)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Post a Comment