Henry, ni balozi wa masomo wa Sky
Aliyekuwa
mshambulizi mahiri wa timu ya Arsenal ya Uingereza na timu ya taifa ya
Ufaransa Thierry Henry aliwashangaza wanafunzi katika shule moja nchini
Wales alipoingia darasani akiwa amevalia nywele bandia na miwani na kuwafunza somo la biashara ya ununuzi.
Wanafunzi
wa shule ya upili ya Pen-y-Dre ilioko, Merthyr walipigwa na bumbuazi
nyota huyo alipojitambulisha kwao kwa niya ya kumkabidhi mmoja wa
wanafunzi wa shule hiyo tuzo la ufanisi katika michezo inayodhaminiwa na shirika la habari la Sky.
Thierry Henry aliwashangaza wanafunzi katika shule moja nchini Wales alipoingia darasani akiwa amevalia nywele bandia na miwani
Thierry Henry aliwashangaza wanafunzi katika shule moja nchini Wales alipoingia darasani akiwa amevalia nywele bandia na miwani
Henry, ambaye ni balozi wa masomo wa Sky alimkabidhi Emma Morgan tuzo hilo kwa mchango wake katika michezo.
Kipindi
hicho cha kuwatuza wanafunzi waliochangia katika michezo katika umri
mdogo kitapeperushwa hewani siku ya jumapili katika Sky Sports1.
Emma
ambaye amethibitisha udedea wake katika uogeleaji aliweka rekodi ya
kuwa mwanafunzi mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuiwakilisha Wales katika
mashindano ya bara ulaya ya uogeleaji huko Sweden.
Emma alimaliza katika nafasi ya pili katika kitengo chake na kutuzwa nishani ya fedha.
Henry alimtuza muogeleaji Emma Morgan
Henry alimtuza muogeleaji Emma Morgan
Muogeleaji huyo atakuwa
miongoni mwa wanaspoti watakaotuzwa siku ya jumapili wakati wa sherehe
ya kumtuza mwanaspoti bora nchini Uingereza Wales na Ireland.
Henry alisema kuwa Emma alikuwa mwenye ari ya kufaulu na hivyo alistahili tuzo hilo.
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo Keith Maher alisema "kila mmoja wetu alikuwa
ameahidi kutotoboa siri hii ya wazo lake Henry mwenyewe kuingia darasani
na
kujitambulisha kama mwalimu mpya wa Biashara ,,,ilikuwa wazo zuri na limeibua muamkompya miongoni mwa wanafunzi.''(BBC)

Post a Comment