Baadhi ya wateja wa nguo wakichagua nguo kwenye soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Miongoni
mwa mambo ya aibu katika jamii ni pamoja na masuala ya udhalilishaji wa
kijinsia ukiwemo ule wa maungoni hasa kwa wanawake.
Kwa
muda mrefu mtandao huu umekuwa ukifuatilia vitendo hivyo vibaya kwa
jamii vinavyofanywa na watu waliokosa ustaarabu hasa jamii ya vijana
katika maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi karibu maeneo mengi ikiwemo
jiji la Dar es Salaam.
Miongoni mwa eneo linaloongoza kwa kuwadhalilisha wanawake ni eneo la soko la Mchikichini lililopo Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.
Mtandao
huu umekuwa ukishuhudia vitendo hivyo vibaya kwa jamii ambapo wengi
wa vijana wamekuwa wakifanya kwa makusudi kuwadhalilisha wanawake hasa
wasichana wadogo kwa kuwashika maungoni (makalio, kifua/maziwa) huku
wakiwalazimisha kununua bidhaa zao.
Vitendo
hivi vimekuwa ni kama mchezo wa kawaida kwani vijana hao wamekuwa
wakiendeleza hali hiyo kwa muda mrefu sasa huku wasichana/wakike hao
wanaofanyiwa vitendo hivyo wakiwa hawana wa la kufanya, Mtandao huu
tunasema huo ni udhalilishaji na unatakiwa kuchukuliwa hatua za haraka
kukomeshwa kwani unakiuka maadili na utu wa mwanamke.

Modewji blog tunatambua
ipo mamlaka husika zinazoweza kulichukulia hatua suala hili basi kama
zipo zianze sasa kwani udhalilishaji huu huko mbele unaweza kuleta
madhara makubwa kwa mtendewa na hata anayetenda kwani akiachwa sasa
baadae anaweza kufanya tukio kubwa na likafumbiwa macho ikiwemo kubaka.
Nachelea
kuamini kama vijana hawa wanafanya hivi kwa kujiamini ama kuna nguvu
ya msukumo nyuma yake? Kipindi cha nyuma sote tumekuwa tukishuhudia
vijana hao wakiwachania nguo wanawake waliokuwa wakivaa vimini waliokuwa
wakipita katikati ya mitaa ya Kariakoo wakati huo huo wamesahau kuwa
nguo hizo wamewauzia wao, tukiacha hilo pia wapo hawa Makondakta wa
daladala nao ni miongoni mwa watu wanaoongoza kufanya vitendo vya
kidhalilishaji wanawake.
Mtandao
huu umeweza kuliona hilo kwa upande wa Makondakta wa Daladala nyingi
hasa nyakati za abiria wa kike anapopanda hatua ya kwanza wao
wanapeleka mkono kwenye ‘Makalio’ ya Mwanamke na kumvutia ndani ya
daladala, yaani kama sapoti ya kumuingiza ndani.
Kondakta
anafanya hivyo wakati huo amekaa mlangoni mwa daladala yake, lakini
anapopanda mwanaume usogea ndani ama hushuka chini bila hata ya
kumshika, lakini akipanda Mwanamke tu utakuta Konda anamshika makalio
kuona kwamba ni jambo la kawaida, Hivyo ni wakati sasa wa kubadilika
jamani vitu vingine hivi ni kushusha utu wa mwanamke hivyo tubadilike na
tuchukue hatua, Asante.
Tuma maoni yakoo hapa kwenye blog hii ama kupitia simu 0719076376

إرسال تعليق