Huku
nusu ya matokeo katika uchaguzi wa rais nchini Nigeria yakiwa
yametangazwa, mgombea kutoka chama kikuu cha upinzani, Muhammadu Buhari,
anaongoza dhidi ya rais aliye madarakani, Goodluck Jonathan.
Lakini
majimbo ya kusini yenye idadi kubwa ya watu kama vile Lagos na Rivers
bado hayajatangaza matokeo na mwandishi wa BBC mjini Abuja amesema
mchuano bado ni mkali.
Tume ya uchaguzi imesema itaendelea
kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne asubuhi na kwamba matokeo ya
mwisho yanatarajiwa kutolewa baadaye siku hiyo. Mwandishi wa BBC anasema
yeyote atakayeshinda, litakuwa jambo la kushangaza iwapo mgombea
atakayeshindwa hatatamka kuwepo kwa mbinu chafu.
إرسال تعليق