WALIMU KUANZISHA BENKI YA BIASHARA MWAKA HUU

Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu  Yahya Mgulwa (kushoto) akizungumza katika kikao hicho.
Wanahabari wakichukua matukio katika kikao hicho.
Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania, Gratian Mukoba (katikati) akitoa tamko la mchakato wa ufunguzi wa benki hiyo.  Pembeni ni viongozi wa CWT.
...Akiendelea kutoa ufafanuzi.
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT) kinategemea kuanzisha benki yake itakayojulikana kama Mwalimu Commercial Bank baada ya kuuza hisa kwa walimu na Watanzania wote tangu Machi 23 hadi Mei 4 mwaka huu.
Hayo yalisemwa leo na Rais wa CWT, Gratian Mukoba, kwa wanahabari na kufichua kwamba benki hiyo inatarajiwa kufungua milango yake Novemba 2 mwaka huu ambapo anategemea itaanza kwa mtaji wa sh. Bilioni 25 kutokana, miongoni mwa mambo mengine, na kivutio cha 50,000/= kutoka kwa kila mwalimu, kiwango ambacho kitamwezesha kununua hisa 100 katika benki yake hiyo.
Alisema maombi ya kuuza hisa za benki ya walimu yameshakubaliwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
 ‘’Ninaomba ieleweke kuwa kama nilivyokwishaeleza hapo awali kuwa tunategemea kuanza kuuza hisa zetu tarehe 23 Machi 2015 na uuzwaji wa hisa hizi utaweza kuchukua kipindi cha wiki sita, baada ya hapo tutapeleka majina ya wanahisa wetu Benki kuu ya Tanzania kwa ajili ya uhakiki na benki yetu kupatiwa leseni yake tayari kwa kuanza biashara, hivyo hisa  zitaorodheshwa kwenye soko la hisa tarehe 8 Juni, 2015,’’ alisema Mukoba.
Kiongozi huyo wa CWT aliongeza kwamba kutokana na idadi ya walimu ambao ni zaidi ya laki mbili nchini,  pamoja na Watanzania wengine, watapata wananchama wapatao laki tatu, hivyo aliwaomba wananchi wajitayarishe kwa ununuzi wa hisa hizo.

Post a Comment

Previous Post Next Post