Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Yahya Mgulwa (kushoto) akizungumza katika kikao hicho.
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT) kinategemea kuanzisha benki yake
itakayojulikana kama Mwalimu Commercial Bank baada ya kuuza hisa kwa
walimu na Watanzania wote tangu Machi 23 hadi Mei 4 mwaka huu.
Hayo yalisemwa leo na Rais wa CWT, Gratian Mukoba, kwa wanahabari na
kufichua kwamba benki hiyo inatarajiwa kufungua milango yake Novemba 2
mwaka huu ambapo anategemea itaanza kwa mtaji wa sh. Bilioni 25
kutokana, miongoni mwa mambo mengine, na kivutio cha 50,000/= kutoka kwa
kila mwalimu, kiwango ambacho kitamwezesha kununua hisa 100 katika
benki yake hiyo.
Alisema maombi ya kuuza hisa za benki ya walimu yameshakubaliwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
‘’Ninaomba ieleweke kuwa kama nilivyokwishaeleza hapo awali kuwa
tunategemea kuanza kuuza hisa zetu tarehe 23 Machi 2015 na uuzwaji wa
hisa hizi utaweza kuchukua kipindi cha wiki sita, baada ya hapo
tutapeleka majina ya wanahisa wetu Benki kuu ya Tanzania kwa ajili ya
uhakiki na benki yetu kupatiwa leseni yake tayari kwa kuanza biashara,
hivyo hisa zitaorodheshwa kwenye soko la hisa tarehe 8 Juni, 2015,’’
alisema Mukoba.
Kiongozi huyo wa CWT aliongeza kwamba kutokana na idadi ya walimu
ambao ni zaidi ya laki mbili nchini, pamoja na Watanzania wengine,
watapata wananchama wapatao laki tatu, hivyo aliwaomba wananchi
wajitayarishe kwa ununuzi wa hisa hizo.
إرسال تعليق