KUFUATIA madai kuwa staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amejifungua, ndugu, jamaa na marafiki kibao walijazana nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar es Salaam juzi Alhamisi ili kumpa pongezi, lakini walipokuta habari tofauti walimvaa na kumlaumu kwa kuwadanganya.
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
Jumatano usiku katika mtandao
wa kijamii wa Instagram, msanii Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu
aliyepata ujauzito mumewe akiwa jela, alitupia picha ikimuonyesha akiwa
na kitoto kichanga, ambacho watu wengi waliamini ni wa kwake, hasa kwa
vile katika siku za hivi karibuni ameonekana kupunguza mitoko.
Watu wa karibu wa muigizaji
huyo ambaye hivi sasa ana uhusiano wa kimapenzi na mcheza shoo wa
Diamond Platnumz aitwaye Iyobo, walikwenda nyumbani kwake kwa ajili ya
kumpongeza, lakini walipatwa na mshangao baada ya kumkuta akiwa na tumbo
lake kama kawaida.
“Sisi tulijua mwenzetu
amejaaliwa kujifungua salama, sasa jambo la kushangaza wenzake tumekuja
kwa furaha tunakutana na mtu mzima kabisa, hivi aliwaza nini kuweka
picha ile katika mtandao na wala asiseme ukweli wa kinachoendelea,”
shoga mmoja wa muigizaji huyo aliliambia gazeti hili nje ya nyumba yake,
lakini akaomba jina lake lihifadhiwe gazetini.
Mmoja wa marafiki waliodaiwa
kufika wakiwa wamekasirika nyumbani kwa Aunt, alikuwa ni shosti yake
Wema Sepetu, aliyeshangaa sababu za kutoambiwa mapema kuhusu ukweli wa
ishu hiyo.
“Nilishtuka kweli, nikasema
inakuwaje Aunt apate mtoto halafu mimi nione kwenye mitandao ya kijamii?
Nafika hapa kumbe hamna lolote Aunt naye hakufanya fair bwana,” alisema
Aunt.Ujauzito wa Aunt kwa sasa unadaiwa kukaribia mwezi wa saba, hivyo
wengi waliposikia amejifungua walidhani amepata kiumbe njiti.

إرسال تعليق