ACT SASA NI JINO KWA JINO,WATANGAZA KUIZUNGUKA TANZANIA,NI KUTANGAZA AZIMIO LA ARUSHA,NA HAPANA YA KATIBA MPYA.


Mwenyekiti wa ACT wazalendo mama ANNA MGHWIRA akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimio ya kamati kuu ya ckama hicho iliyoketi jana
Baada ya kufanya uchaguzi wa chama na uzinduzi wa chama kwa mafanikio makubwa chama kipya cha ACT-wazalendo nchini tanzania leo kimetangaza kuanza kuishambulia mikoa kadhaa nchini kwa lengo la kutangaza azimio la arusha baada ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho kuamua kufanya hivyo.

AkizUngumza na wanahabari mapema leo mwenyekiti wa ACT wazalendo mama ANNA MGHWIRA amesema kuwa kamati kuu ya chama imeamua kuanza ziara ya ambayo ni ziara ya kwanza na kupita katikia mikoa takribani kumi yenye lengo la kutangaza azimio la arusha lililiuhishwa baada ya kupitishwa na vikoa vya chama ambapo amesema kwa sasa azimio hilo lipo katika hatua ya kuchapishwa.

Ziara hiyo ambayo itawahusisha viongozi wakuu wa chama itapita katika mikoa ya Ruvuma,njombe,iringa,morogoro,Dodoma ,singida,tabora,shinyanga,mwanza na mara,ziara ambayo amesema kuwa inatarajiwa kuwa na mafanikio makubwa katika chaka kutokana na mapokeo ya chama hicho kuwa ni makubwa kwa watanzania.

Aidha katika hatua nyingine chama hicho kimeungana na vyama vya UKAWA pamoja nna wanaharakati mbalimbali ambao kwa pamoja wamekuwa wakipinga mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya ambapo kamati kuu ya chama hicho nayo imetangaza rasmi kuwahamasisha watanzania pamoja na wanachama wa chama hicho kuipigia kura ya hapana katiba inayopendekezwa kutokana na kile walichokiita ni ubatili wa mchakato mzima wa kupatikana kwa katiba hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post