Mwenyekiti wa
Wafanyabiashara Nchini, Johnson Minja ameachiwa kwa dhamana na serikali
imeambiwa isisikie maneno ya kuambiwa.
Mwenyekiti huyo ambaye alifutiwa
dhamana Machi 26, alirejeshwa mahakamani leo ambapo kesi yake ilitajwa,
akitokea gereza la Isanga.
Kwa mujibu wa mahakama ya
mkoa wa Dodoma, kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa maelezo ya awali Aprili 9
mwaka huu kutokana na ushahidi wa kesi hiyo kukamilika.
Machi 5, mwaka huu,
Mahakama ilimuonya mshitakiwa huyo kuacha kuwashawishi
wafanyabiashara nchini
kuacha kufunga maduka yao na kwenda kusikiliza kesi
yake kila inapotajwa.
“Moja ya sharti la dhamana yako ni kuhakikisha
kuwa unaendeleza amani
wakati wote wa kesi yako
ikiwa ni pamoja na kuwaambia wafanyabiashara
waendelee kufungua maduka
yao ili wananchi waendelee kupata huduma, kwanini
umewaambia wafanya
biashara wafunge maduka yao?” alihoji hakimu Mbilu.
Hata hivyo Minja alijibu
kuwa hana taarifa zozote za wafanyabiashara nchini
kufunga maduka.
Walisema wanasuburi leo
kama mwenyekiti huyo ataashiwa tena kwa dhamana ili
waendelee na biashara
kwani wengi wao wana mikopo ya benki na wamekaa wiki
nzima bila kufanya
biashara.
Post a Comment