Siku Ya Wajinga (April Fool) Na Hukumu Yake Kishari’ah

Habari wasomaji wa mtandao huu wa Modewji blog, munaoendelea kuperuzi, Leo ni Aprili Mosi, ambapo kila mwezi wa nne tarehe moja kama ya leo Duniani kote watu mbalimbali huifaanya siku hii kama ni ya kutaniana na kufanya jambo la mzaha ama ujinga ambalo ufanywa kuanzia tarehe inapoanza hadi saa nne asubuhi.
Hata hivyo siku hii ya wajinga kwa kipindi hiki imezidi kuwa na nguvu hasa baada ya kuongezeka mitandao ya kijamii ambayo watu mbalimbali wanaooitumia kutumia wasaha wa kuposti taarifa za uongo na uzushi huku wengine wakienda mbali na haataa kubandika picha za ku-edit ilimradi tu aonekane ni mkweli.
Hatahivyo wapo wanaofanya hivi pasipokujulisha mwisho wa taarifa yake hiyo kama ni siku ya wajinga na wapo wanaofanya hivyo kuajulisha ni siku ya wajinga na mambo kama hayo.
Mtandao huu tunakuletea makala maalum ambayo inaelezea siku hiyo wa wajinga duniani ambayo pia imeelezea na namna na suala la kiimani inavyoweza kuwa baya. .

                                                                                      Uzushi na Maovu
aprilfool
Muhammad Baawazir
بسم الله الرحمن الرحيم 
BismiLLaah walhamduliLLaah Rabbil ‘Aalamiyn. Was-Swalaatu was-Salaamu ‘alaa Nabbiyihi asw-Swaadiq Al-Amiyn, wa ‘alaa aalihi wa Swahaabatihi al-Ghurr Al-Mayaamiyn, wa man Tabi’ahum bi Ihsaani ilaa Yawmid Diyn.
Amma ba’ad: 
ASILI YA APRIL FOOL 
Asili ya April Fool haikujulikana kwa uhakika na kuna rai mbali mbali zinazohusiana nayo.
Wengine wamesema imeanza kutokana na sherehe za majira ya kuchipua (Spring) katika ikwinoksi (siku ya mlingano) tarehe 21 Machi.
Wengine wamesema kuwa huu ni uzushi uliochomoza France mwaka 1564 M, baada ya utangulizi wa kalenda mpya. Wakati mtu alipogoma kukubali kalenda mpya akaishia kuwa ni mwathirika wa baadhi ya watu ambao wamemsababisha aathirike kufedheheka na wakamfanyia istihzai na kumtania, akawa ni kichekesho kwa watu.
Wengine wanasema kuwa uzushi huu umeanza asili yake katika nyakati za kale na sherehe za mapagani zilikuwa na uhusiano na siku hasa mwanzo wa majira ya kuchipua. Kwa hiyo hii ni kasumba ya ibada za mapagani. Inasemekana kuwa nchi nyingine, kuwinda hakukufaulu siku za mwanzo za uwindaji.
Le poisson d’avril (Samaki wa Aprili)
Wazungu wameiita April Fool kwa jina la ‘le poisson d’avril’ (Samaki wa Aprili). Na sababu hii ni kutokana na jua linavyosogea kutoka nyumba ya zodiaki (nyota za unajimu) ya Pisces (Nyota ya samaki) ikielekea nyumba nyingine. Au kwa sababu ya neno la poisson ambalo maana yake ni samaki, hivyo ni ugeuzaji wa neno la ‘passion’ ambayo ina maana ya ‘kuteseka’. Kwa hiyo ni alama ya kuteseka aliyovumulia Nabii ‘Iysa (Alayhis Salaam) kama walivyodai Wakristo. Na madai yao haya yalitokea wiki ya kwanza katika mwezi wa April.
Baadhi ya makafiri wameiita siku hii ‘Siku nzima ya wajinga’ kama inavyojulikana Kingereza. Hii ni kwa sababu uongo wanaousema ili wale wanaousikia waamini kwa hiyo wanakuwa ni waathirika wa wale wanaowafanyia dhihaka.
Utajo wa mwanzo kabisa kwa Lugha ya Kingereza ilikuwa ni katika gazeti la Dreck. Siku ya pili ya Aprili 1698 M, gazeti hili lilitaja kwamba idadi kadha ya watu walialikwa kuhudhuria uoshaji wa watu weusi katika mnara wa London asubuhi ya siku ya mwanzo ya Aprili.
Tukio maarufu kabisa lililotokea Ulaya tarehe 1 Aprili lilikuwa wakati gazeti la Kingereza ‘Evening star’ lilipotangaza mwezi wa Machi 1746 M kwamba siku ya pili tarehe 1 Aprili, kutakuwa na gwaride la punda mji wa Islington Uingereza. Watu wakakimbilia kuwatazama wanyama hao na kulikuwa na zahma kubwa. Wakaendelea kusubiri na walipochoka kusubiri, waliuliza kutaka kujua hili gwaride litakuweko baada ya muda gani. Hawakupata jibu, hivyo wakatambua kuwa wamekuja kufanya maonyesho yao wenyewe kama kwamba wao ndio mapunda.
Mmoja wao ameandika kuhusu asili ya uzushi huu kwa kusema: Wengi wetu tunasherehekea siku inayojulikana kuwa ni April Fool, au ikiwa itafasiriwa kihalisi ‘Siku ya Ujanja’. Lakini je, tunajua siri chungu inayohusikana na siku hii?
Habari nyingine ambazo usahihi wake umetiliwa shaka na wanahistoria ni kuwa:
Waislamu walipotawala Hispania (Spain) takriban miaka elfu iliyopita, kulikuwa na nguvu kubwa ya utawala wa Kiislam ambayo haikuwezekana kuivunja. Wakristo wa Kimagharibi walitamani kuufuta Uislamu katika mgongo wa ardhi na walifaulu kwa kiwango fulani.
Walijaribu kuzuia Uislamu kusambaa Hispania na walitaka kuuzima na wautoweshe kabisa lakini hawakufaulu, ingawa walijaribu mara nyingi bila ya kufaulu.
Baada ya hapo, makafiri walituma majasusi Hispania kufanya utafiti ili kujua siri ya nguvu za Waislamu ambayo haikuwezekana kuishinda. Wakatambua kuwa kushikamana na Taqwa (Ucha Mungu) ndio sababu.
Wakristo walipotambua siri ya nguvu za Waislamu, wakaanza kufikiria mikakati za kuvunja nguvu hiyo. Na kwa ajili hii wakaanza kupeleka ulevi na sigara bure huko Hispania.
Mbinu hizi kwa upande wa Magharibi zilifaulu kuleta taathira na imani za Waislamu zikaanza kulegea, hasa miongoni mwa vizazi vipya Hispania. Matokeo yake ni kwamba Wakristo Wakatholiki waliikandamiza Hispania nzima na wakauangamiza utawala wa Kiislamu katika ardhi hiyo, utawala ambao ulidumu zaidi ya miaka mia. Ngome ya mwisho ya Waislamu Grenada ilianguka tarehe 1 Aprili, hivyo wakaichukulia kuwa ni ‘Siku ya Ujanja ya Aprili’ au ‘Siku ya Wajinga ya April’.  Ujanja kwa wale walioufanya, na Ujinga kwa wale waliofanyiwa na kutumbikia ndani yake.
Tokea mwaka huo hadi sasa, wanasherehekea siku hii na wanachukulia kuwa Waislamu ndio wajinga. Hawakuuhusisha ujinga huu na jeshi la Granada pekee kuwa ni wajinga, bali wamekusudia kuwa ni Umma wa Kiislamu mzima kuwa ni wajinga.
Hata hivyo, habari hizi tumezinukuu hapa kwa kuwa zimeenea sana miongoni wa Waislam, lakini kama tulivyotangulia kueleza, ni kuwa, uhakika na ukweli wake una mashaka kwa sababu kuna wanaosema kuwa wakati huo sigara na uvutaji tumbaku ulikuwa haujaanza hadi baada ya kushindwa Waislamu huko Hispania. Wahahistoria wanasema sababu za kushindwa Waislamu zilikuwa ni wenyewe kujiingiza zaidi kwenye mapenzi ya kidunia na starehe, pamoja na kuacha mafundisho sahihi ya Uislam na badala yake kuchanganya zaidi na falsafa ya Kigiriki na kutegemea zaidi fikra za kirumi katika kuendesha mambo yao badala ya mwongozo imara wa Kiislam. Kadhalika kuna Waislamu waliokuwa wakishirikiana na makafiri katika kupambana na makundi mengine ya Kiislam waliyokuwa hawaelewani nayo kama tunavyoona leo hii.


 BAADHI YA UDANGANYIFU WANAODANGANYANA WATU KATIKA
SIKU HII YA APRIL FOOL

Wengine wanapewa habari ya mmoja wa kipenzi chake katika familia kama mtoto, mke au mume kwamba amefariki na kwa wengine taarifa hizo husababisha hata kifo chao kutokana na kutokustahamili kupata mshtuko huo. Wengine wanapewa habari ya kufukuzwa kazi, au kuwashtua kwa habari mbaya kama kuunguliwa moto nyumba yake, au familia yake kupata ajali, na husababisha aathirike mtu kwa mshtuko huo hadi apate maradhi ya moyo, au maradhi ya kupooza au hata kifo cha ghafla. 
  Kusoma zaidi bonyeza hapa: http://www.alhidaaya.com/sw/node/3859

Post a Comment

Previous Post Next Post