Gazeti moja nchini Ujerumani na
jarida la Ufaransa yameripoti kuwa yameona picha za video zilizopigwa
kwa simu zinazoonyesha dakika za mwisho ndani ya ndege ya Germanwings
iliyoanguka katika milima ya Alps wiki iliyopita. Picha hizo za video
zinadaiwa kuwa zilipatikana kwenye programu ya kuhifadhi kumbukumbu
yaani memory-card iliyopatikana eneo la tukio. Katika picha hizo abiria
ndani ya ndege hiyo wanaonekana wakipiga kelele huku sauti ya rubani na
jitihada za kutaka kufungua mlango ili aingie kuokoa ndege hizo
zikisikika. Rubani msaidizi wa ndege hiyo, Andreas Lubitz,anayeaminika
kuwa ndiye aliyesababisha ajali hiyo alikuwa ndani ya chumba cha ndege
huku akiqwa amefunga mlango mwenzake asiingie
Post a Comment