ALA PASAKA KWA KICHAPO

Kijana mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Anton, Jumapili ya Pasaka alikula sikukuu kwa kupewa kichapo na wananchi wenye hasira kwa madai kuwa ni kibaka.Tukio hilo lililotokea saa 12 asubuhi maeneo ya Sinza Afrikasana ambapo walioshuhudia tukio hilo walimwambia mwandishi wetu kuwa, kijana huyo aliyefahamika mtaani hapo kama muokota chupa, ilidaiwa kuwa  alikurupushwa kutoka katika nyumba moja ambako alienda kwa gia ya kuokota chupa, akataka kukwapua kitu.
Anton akivuja damu baada ya kupewa kichapo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira kali kwa kosa la wizi.
“Baada ya kukurupushwa katika nyumba hiyo, kijana huyo alitoka mkuku mpaka katika nyumba moja ambako alimkuta dada mmoja akifagia na kuingia ndani ya geti  kisha kujifungia,” alisema shuhuda mmoja.
Baada ya muda wakatokea watu waliomkurupusha ndipo dada huyo akawaambia kuwa mtuhumiwa wao ameingia ndani baada kulikuta geti hilo wazi wakati akifanya usafi na alikuwa amejifungia kwa ndani.
Habari hiyo iliwafanya baadhi ya vijana kudandia geti ili kuingia ndani, hata hivyo, kijana huyo alipoona watu hao wakiruka getini naye akaruka ukuta upande wa pili na kukimbia.
Akipakizwa kwenye gari safari kuelekea kituoni.
Lakini juhudi zake hizo za kutaka kutoroka hazikuzaa matunda kwani alidakwa hatua chache kutoka kwenye ukuta wa ua wa nyumba hiyo na kuanza kula kichapo kikali ambacho kilisababisha kuchanwa kichwani na damu nyingi ‘kumwagika.’
Kijana huyo aliokolewa na askari polisi waliokuwa doria wakiongozwa na Kamanda Rashidi wa Kituo cha Polisi Mabatini waliokuwa katika gari yao ya doria.
Moja ya jeraha kubwa alolipata kichwani baada ya kichapo.
Kamanda huyo na askari wenzake walifanya kazi kubwa kuzuia raia wasilete madhara zaidi kwa kijana huyo huku wakiwaambia wananchi kuwa siyo busara kujichukulia sheria mkononi, walimkamata wakampeleka kituoni kwa hatua zaidi

Post a Comment

أحدث أقدم