TAMAA ya kutaka Sikukuu ya Pasaka iwe nzuri kwa kufanya matanuzi kwa
pesa za kuzipata kirahisi pasipo kutoka jasho, wiki iliyopita zilimponza
kijana mmoja ambaye jina lake halikupatikana, baada ya kujikuta
akichezea kichapo ‘hevi’ hadi kuvunjwa miguu, baada ya kujaribu kuiba
baiskeli katika Soko la Mwembe Chai, lililopo Magomeni jijini Dar es
Salaam.
Mwizi baada ya kupokea kichapo toka kwa wananchi.
Kijana huyo mkazi wa Magomeni Makuti, Dar inadaiwa alipita sokoni
hapo akiwa katika mihangaiko yake ya kawaida, kabla ya kuiona baiskeli
hiyo iliyompa kishawishi cha kuikwapua. Baada ya kuichukua na kuanza
kuendesha, hatua chache mbele yake, pedeli moja ilichomoka, kitendo
kilichomfanya ashuke na kuanza kukimbia kuogopa wananchi ambao
walishaanza kumpigia kelele za mwizi.
Hata
hivyo, hakufika mbali alizingirwa na wananchi ambao walianza kumpa
kipigo, inadaiwa kuwa kijana huyo aliomba asamehewe kwa vile
kilichomfanya akwapue baiskeli ni kutaka kupata pesa kwa ajili ya
Sikukuu ya Pasaka itakayoadhimishwa Jumapili hii.
Katika
kipigo hicho, mmoja wa madereva wa pikipiki alimkanyaga miguuni na
kumvunja jambo lililompa maumivu makali na kumfanya azimie kabla ya
wasamaria wema kuwaita polisi wa Kituo cha Magomeni ili kumnusuru kibaka
huyo
Post a Comment