Kukubali! Baba mzazi wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Abdul Jumaa ‘Baba D’ amefunguka kuwa, kwenye listi ya
wanawake wote waliowahi kuwa na mwanaye kimalovee, mwanadada Zarinah
Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ndiye mkwe wa ukweli kwake kutokana na kuwa
tayari kumletea mjukuu.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mpenzi wake Zarinah Hassan 'Zari'.
Akizungumza na Amani, juzikati jijini Dar, baba Diamond alisema kuwa
miongoni mwa vitu ambavyo vilikuwa vikimkosesha amani ni maneno
yaliyokuwa yakimsakama Diamond kuwa huenda hana uwezo wa kumpa mimba
mwanamke, kiasi cha warembo wote aliowahi kuripotiwa kutoka nao kutoka
patupu bila kushika ujauzito.
“Nawashangaa sana hao wanawake si huyo Wema (Sepetu) wala hao
wenziye, maana Diamond alisema kampa mimba Penny (Penniel Mungilwa)
zikatoka huku mwenyewe akikanusha hajawahi kushika mimba kwa kumchafua
tu mwanangu aonekane siyo mwanaume rijali,” alisema mzazi huyo.
Baba mzazi wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa ‘Baba D’.
Baba D alitiririka kwamba mastaa hao wa kike ambao Mbongo Fleva huyo
aliwahi kutoka nao huenda wao ndiyo hawana kizazi hivyo wanamtupia
lawama mtoto wake kwa kushindwa kuwazalisha.
Alisema kuwa kikubwa anachokiamini wote hawakuwa na upendo wa kweli
kwa mwanaye, walitaka kuzitumia tu fedha zake na kumuacha solemba lakini
sasa Zari ndiye mwenye penzi la dhati kwa mwanaye.
“Kiukweli Zari kanifurahisha. Ndiye mkwe wangu wa kweli na halali kabisa.
“Nampongeza sana Zari kwa kushika ujauzito wa mwanangu. Sasa Diamond atatembea kifua mbele kwa kujiamini,” alisema baba D.
Alisema kutokana na kile kilichokuwa kikiaminika kuwa hana maelewano
mazuri na mkali huyo wa Bongo Fleva, kwa sasa wapo vizuri na hata akiwa
na tatizo huwa anamwambia Diamond ambaye amekuwa akimpa msaada.
“Kwa sasa nina maelewano mazuri na Diamond, muda wowote nikiwa na
tatizo huwa namjulisha ananisaidia, kitu ambacho kinamfanya amgharamie
mama yake kuliko mimi ni kwa sababu aliishi naye kwa kipindi kirefu na
kuhangaika naye tangu utotoni,” alisema.
Ukiacha Zari ambaye amekubali kubeba ujauzito wake, Diamond aliwahi
kuwalalamikia baadhi ya wapenzi wake kuwa walikataa kumzalia mtoto
akiwemo Wema, Penny na Jokate Mwegelo.
Post a Comment