Bruce
Jenner aliyekuwa mwariadha bora duaniani kabla ya kuwa nyota wa kipindi
cha televisheni na familia moja maarufu duniani ''The Kardashians''.
sasa amefichua siri ambayo amekuwa akiificha kwa miaka mingi.
''Kwa
nia na madhumuni yote, mimi ni mwanamke.'' Jenner aliambia Sawyer
kutoka ABC katika mahojiano maalum yaliopeperushwa hewani siku ya
Ijumaa.
''Watu wananiona tofauti,wananiona kama mwanaume, lakini
moyo na roho yangu na kila kitu ninachofanya maishani ni sehemu yangu.''
Jenner ambaye ana umri wa miaka 65 amesema. '' Upande huu wa kike ni
sehemu yangu.
hivi ndivyo mimi nilivyo.''
Katika masaa ya mahojiano na
Diane Sawyer mjini New York na California, Jenner alielezea kwa kina
mapambano yake ya kuwa na jinsia mbili tangu utotoni.
''Akili
zangu ni za kike sana kuliko za kiume.'' Ameongezea. '' Ni vigumu sana
watu kuelewa, lakini hivyo ndivyo nafsi yangu ilivyo.''
Jenner
aliyejawa na hisia na mwenye nywele ndefu shati na suruali ndefu alisema
kuwa amesubiri kwa miaka mingi ili kujitangaza kwa kuwa hakutaka
kuwavunja moyo watu.
Kwa miongo kadhaa wake wa zamani wa Jenner na
madada zake waliweka siri kuhusu jinsia yake na kwamba walikuwa watu
waliokuwa wakijua siri hiyo.
Mtandao wa watu wanaojua siri hiyo hatahivyo ulipanuka hivi majuzi wakati Jenner alipomwambia mamaake na wanawe 10 .
Jenner
ana watoto sita Burt,Cassandra,Brabdon,Brody,Kendall na Kylie pamoja na
watoto wanne wa kambo akiwemo Kourtney,Kim,Khloe na Rob Kardashian.
إرسال تعليق