CHAMA
 Cha Mapinduzi (CCM), Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kimeanza 
kulisaka Jimbo la Moshi Mjini kwa kutumia helikopta (chopa) ili kiweze 
kuibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi Mkuu ujao.
Katika
 mkutano wao wa hadhara uliofanyika jana kwenye Viwanja vya Soko la 
Pasua, Kata ya Bomambuzi, kada wa chama hicho Buni Ramole kwa jina 
maarufu 'Buni', alitumia usafiri huo kufika eneo la mkutano.
Akihutubia
 mamia ya wanachama wa CCM na wananchi walioshiriki mkutano huo, Ramole 
alisema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepoteza sifa ya 
kuendelea kuliongoza jimbo hilo hivyo kinapaswa kukaa pembeni.
Alisema
 umefika wakati wa CCM kuliongoza jimbo hilo ili kuwaletea wananchi 
maendeleo baada ya jimbo hilo kushikiliwana mbunge wa CHADEMA kwa 
vipindi vitatu mfululizo.
"Naomba
 niwaeleze kuwa, jimbo hili kuongozwa na mbunge wa CHADEMA, Bw. Philemon
 Ndesamburo kwa vipindi vitatumfululizo...katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu
 lazima lirudi CCM, upinzani hawajafanya kitu zaidi ya kusababisha 
mateso kwa wananchi, sasa watupishe," alisema.
Aliongeza
 kuwa, mwaka 2010 wakati Bw. Ndesamburo alikupata ridhaa ya wananchi 
aweze kuliongoza jimbo hilo kwa awamu ya tatu, aliahidi mambo mengi.
Mambo
 hayo ni pamoja na kufungua viwanda vilivyofungwa katika Mji wa Moshi 
lakini hadi sasa ameshindwa kuitekeleza ahadi hiyo hivyo ni wazi kuwa 
aliwadanganya wananchi.
Kada
 huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, alisema CCM kimejipanga vizuri 
kuhakikisha kinalichukua jimbo hilo kwa ushindi wa kishindo ambapo moja 
ya mambo ambayo chama hicho kitafanya baada ya kushinda ni kuwaletea 
wananchi maendeleo na kufungua viwanda vyote vilivyofungwa.
"Jambo
 lingine ambalo tutalifanya ni kata zote za Mji wa Moshi, kuunganishwa 
na barabara za viwango vya lami,nitashirikiana na watendaji wa chama 
changu kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindo...tutaendelea kutumia 
chopana kupita kila kata ili tuweze kuwafikia wananchi wote ili 
kuwaeleza ahadi zetu," alisema.
Akizungumzia
 hatua ya Bw. Ndesamburo kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimbo hilo 
na nafasi hiyo kumpa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Bw. Japhary 
Michael, alisema inaonesha kuwa CHADEMA hakina demokrasia.
"Hivi
 karibuni Ndesamburo alitangaza kuachia ubunge na kumkabidhi mikoba yake
 Japhary Michael, hii inaonyesha wazi kuwa chama hicho hakina demokrasia
 bali ni sawa na SACCOSya mtu anayeweza kuitumia atakavyo," alisema.
Ramole ni mmoja wa makada wa CCM ambaye ametangaza nia ya kutaka kuwania ubunge wa jimbo hilo muda ukifika.
Mwaka
 2010, Ramole alikuwa mmoja kati ya wagombea tisa ndani ya CCM 
waliojitokeza kuwania ubunge wa jimbo hilo ambapo baada ya kupigiwa 
kura, alishinda na kushika nafasi ya kwanza akipata kura 1,554.
Nafasi
 ya pili ilishikwa na Bw. Thomas Ngawaiya aliyepata kura 1,539 ambapo 
Justine Salakana alishika nafasi ya tatubaada ya kupata kura 1,152.
Licha
 ya Ramole kuongoza katika kura ya maoni, jina lake lilienguliwa na 
chama hicho ambapo Salakana aliyeshika nafasi ya tatu, ndiye 
aliyepeperusha bendera ya chama hicho kwa tiketi ya CCM lakini 
hakufurukuta kwa Bw. Ndessamburo.

Post a Comment