Weekend iliyopita Escape One kulifanyika
 show iliyowakutanisha mastar wakubwa ndani na nje ya TZ kama Christian 
Bella, Ruby, Ali Kiba, Kassim Mganga, Ommy Dimpoz, Msami, na Alicious 
kutoka Kenya, Wote kwenye stage moja.
  
Moja ya hits ambazo zimependwa SANA ni ‘Nani Kama Mama‘- collabo ya Ommy Dimpoz na Christian Bella.
  
Soudy
 Brown alikuwa mmoja ya watu waliokuwa kwenye show hiyo Escape 1, 
akamuona Ommy akitokwa machozi wakati wanaimba wimbo huo kwenye stage.. 
Ommy akashindwa kuendelea akashuka, Soudy akamfuata kujua tatizo ni 
nini?
  
Dimpoz 
 amesema aliandika wimbo huo kwa sababu ya kumbukumbu ya kifo cha mama 
yake aliyefariki miaka 15 iliyopita, alimuacha akiwa mdogo sana.. wakati
 anaimba wimbo huo alikumbuka mapenzi ya mama akatamani kama mama yake 
angekuwepo.. ni hicho tu kilichomtoa machozi.

Post a Comment