Mshambuliaji wa Stand United, Haruna Chanongo.
MSHAMBULIAJI wa Stand United, Haruna Chanongo, amepigwa ‘stop’ kwenda kufanya majaribio kwenye kikosi cha timu ya TP Mazembe kutokana na kocha wa timu hiyo kuwa bize kwa sasa.
Chanongo amekuwa katika mipango ya muda mrefu ya kwenda kwenye
majaribio kwenye timu hiyo, lakini juzi alifunguka kuwa hawezi kwenda
kwa sasa kwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo yupo bize na timu hiyo
akiiandaa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza na Championi Jumatano, Chanongo alisema TP Mazembe
imemzuia kwa muda kwenda katika majaribio ya kucheza soka la kulipwa
katika timu hiyo na itampa taarifa baadaye.
“Mipango yangu ya kwenda kufanya majaribio Klabu ya TP Mazembe bado
ipo ila kwa sasa nasubiri kwa muda kidogo kwanza kwani niliambiwa kocha
wa timu hiyo, bado yupo bize kuwanoa nyota wake ambao wanashiriki Ligi
ya Mabingwa.
“Nimeelezwa kuwa muda utakapokuwa tayari nitapewa taarifa niende
lakini sasa naendelea kuitumikia timu yangu ya Stand United kwa nguvu
zote ili kuona inafanya vizuri,” alisema Chanongo
إرسال تعليق