TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CUF Chama cha wananchi kinaona
kinaona dalili kwamba serikali ndio wanachochea migomo nchini kwa kupuuza na
kuchukulia kirahisi sana madai ya wananchi.Mfano mzuri ni mgomo ulifanyika leo
wa madereva kusababisha adha kubwa ya usafiri kwa wananchi mbalimbali nchini
hasa wakazi wa jiji la Dar es salaam.
Usumbufu wa wanachi leo kushindwa
kusafiri na kukakaa vituoni kwa muda mrefu ungeweza kuepukika kama serikali
ingekuwa na utaratibu wa kutosubiri migomo ili kutatua malalamiko ya wananchi
wake.
Tunaitaka tena serikali kumaliza
mgomo huu kwani inawezekana kabisa ikiamua kukaa chini na madereva na
kusikiliza kilio chao bila kutumia mabavu ya dola kwa kuwakamata.Suala la kutaka
mikataba ya ajira wanayodai madereva ni la siku nyingi na serikali imeziba
masikio.Suala la mikataba ya ajira si kwa madereva tu limeenea hata kwa wananchi
mbalimbali kwa kufanyishwa kazi bila
mikataba ya na katika mazingira ya
kunyanyaswa na serikali kufumbia macho.Serikali inasubiri na hayo makundi
mengine yagome?
CUF tuanaitaka serikali kipindi
inawabana madereva ili kupunguza ajali za barabarani pia itazame jinsi barabara
nyembamba inazojenga zinavyochangia kusababisha ajali barabarani.
CUF tunawasihi madereva kusitisha
mgomo wao kwani wananchi wanateseka sana kwa kukosa usafiri. Madereva wanaweza
kutumia njia nyingine nyingi kudai madai yao bila kuwaumiza wananchi.
HAKI
SAWA KWA WOTE
Abdual Kambaya
Naibu Mkurugenzi Habari na
Uenezi, CUF Taifa.
0719566567
إرسال تعليق