Tukio
hilo lilimfanya Davido aandike mfululizo wa tweets za mafumbo ambazo
wengi waliamini kuwa ni madongo kwa Diamond aliyewahi kumshirikisha
kwenye remix ya Number One iliyotokea kuwa hit namba moja Afrika katika
kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Davido na Diamond Platnumz akiwa studio mwishoni mwa mwaka juzi.
Uhusiano
kati ya Davido na Diamond Platnumz ulishavunjika siku nyingi kufuatia
issue iliyotokea mwaka jana kwenye fainali za shindano la Big Brother
Africa.
Kambi
ya Diamond ilisisitiza kuwa hakuna ugomvi kati ya mastaa hao wawili na
hata staa huyo wa ‘Nasema Nawe’ hivi karibuni aliwahi kuupa shavu wimbo
mpya wa Davido kwenye Instagram.
Lakini
vipi kama kweli Davido na Diamond bado ni washkaji? Kwa kile
alichokipost Davido kwenye ukurasa wake wa Facebook, huenda wawili hao
wakawa wanaendelea kupanga kufanya makubwa baadaye.
Kupitia
ukurasa wake wa Facebook, Davido amepost picha ya zamani akiwa na
Diamond kwenye studio yake nchini Nigeria. Kwenye picha hiyo, Davido
ameandika: I think I just recorded a sweeter love song than AYE .. Hmm
this album yo.”
Picha
hiyo imevutia comments nyingi japo asilimia kubwa ni za wakenya
wanaomnyeshea mvua ya matusi! Yes, Wakenya hawataki kumsikia tena
Davido!
Hakuna
shaka kuwa staa huyo wa Nigeria ana picha nyingi ambazo angeweka
kuambatanisha na ujumbe huo. Hivyo, uchaguzi wa picha akiwa na Diamond
unaweza ukawa na dhumuni maalum!

Post a Comment