Msanii wa kitambo katika tasnia ya filamu Bongo, Mayasa Mrisho
‘Maya’, amefunguka kuwa anahisi yeye na mwigizaji mwenzake ambaye ni
mkongwe, Blandina Chagula ‘Johari’ wana gundu kwani wasanii wenzao wengi
wana watoto na wengine ni wajawazito lakini wao wapowapo tu.
Mwigizaji mkongwe Blandina Chagula ‘Johari’.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Maya alisema kuwa kuna
wakati anakaa na kufikiria sana hatma yao na kuona kwamba kama
imeshindikana kuolewa basi wapate hata watoto angalau nao wajidai kama
wenzao.
Msanii wa kitambo katika tasnia ya filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’.
“Mimi na Johari ni wasanii wakongwe sasa sijui ni gundu ama nini,
kama hatupo kwenye listi ya wale wa kuolewa basi tupate hata mtoto
mmojammoja maana mimi naona tunazidi kuzeeka kabisa kila siku inayoenda
kwa Mungu,” alisema Maya.
إرسال تعليق