Wachimbaji wadogo wadogo 19 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mvua
hizo zimesababisha kubomoka kwa mashimo katika machimbo ya kijiji cha
Karore kata ya Runguya tarafa ya msalala wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo.
Wachimbaji hao wanadaiwa kuvamia machimbo hayo ambayo yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu, wakaanza shughuli ya uchimbaj
Post a Comment