Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akimsikiliza kwa makini Mwakilishi
Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe
Dongier walipokutana katika mikutano hii ya kipupwe inayoendelea hapa
Mjini Washington DC.Wengine ni ujumbe kutoka Tanzania pamoja na timu ya
wataalam kutoka Benki ya Dunia.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum akifuatilia kwa makini maswalialiyokuwa
akiulizwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda
na Burundi Bw. Philippe Dongier hayupo kwenye picha. Kulia ni katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Bw.
Ujumbe
wa Mkutano huo kutoka pande zote mbili yaani Tanzania na Benki ya
Dunia, wakimsikiliza kwa makini Mchumi mwandamizi kutoka Benki ya Dunia.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile akijadiliana jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia
Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier kabla ya kikao
kuanza rasmi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile akiandika kwa makini hoja na mapendekezo yaliyokuwa yakitolewa
na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na
Burundi Bw. Philippe Dongier.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile akijibu na kueleza kwa umakini hoja na mapendekezo yaliyokuwa
yametolewa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda,
Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
…………………………………………………
Wakati
Tanzania ikiendelea kupambana na umaskini , Benki ya Dunia imesema
kuwa,” tumefurahishwa sana na mwenendo mzuri wa usimamizi wa fedha na
bajeti”. Hayo yalisemwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania,
Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier katika mkutano ambao
waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum alikuwepo.
Mambo
mbalimbali yalizungumziwa katika mkutano huo ambapo suala la
upatikanaji wa fedha kusaidia bajeti ya serikali
lilipewakipaumbele.Maboresho katika Sekta ya umeme nalo jambo mojawapo
liliopewa uzito kwani Nchi wahisani wamepata moyo wakuachia misaada
baada ya kuona Serikali imeweza kulishughulikia suala zima la IPTL.
“
Nchi wahisani wamekubali kuendelea kutoa misaada kwa asilimia mia, hii
ni kwa sababu tu! serikali yenu imekubali kuchukua hatua dhidi ya tatizo
la IPTL”, alisema Philippe.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mhe. Mkuya alisema kuwa, suala la kuboresha
Pension nalo lilizungumziwa na chombo hiki kitasaidia serikali katika
kuboresha malipo ya uzeeni (pension) na kuwezesha mashirika ya “pension”
ili yaweze kuwa na uwezo wa kusaidia wastaafu. Aidha tumekubaliana kuwa
watatusaidia katika suala zima la kuboresha uwazi serikalini na
mazingira ya biasha Tanzania.Aliongeza Mkuya.
Jambo
lingine lililochukua uzito katika majadiliano hayo ni suala la kufanya
ukaguzi Bandarini. Hili limejitokeza baada ya kubainika kuwa kuna baadhi
ya wafanya biashara sio waaminifu hivyo benki ya Dunia imeitaka
Serikali kuangalia upya maamuzi ya mwanzo ya serikali yakuto kagua
mizigo, na kusema kuwa wanasubiri majibu juu ya kubadilisha utaratibu wa
mwanzo. Tanzania imekubali kukaa kwa pamoja Wizara na Fedha na TRA ili
kurudisha majibu na mkakati ambao kama serikali watakuwa wamekubaliana.
“Kumekuwa
na madai mengi ambayo yanadaiwa na makandarasi na wafanyabiashara
wadogo, tutajitahidi kuyalipa iliyaishe lakini kwa wale wenye nyaraka
halali, tunaenda kupiga marufuku kwa Afisa masuuli wote kuwa kuanzia
sasa hakuna kufanya malipo yoyote kama hakuna fedha kwa ajili ya
shughuli hiyo”.Alisema Mkuya.
“ Hii itasaidia kupunguza madeni. Ninasema haya kwani ndicho kitu tulichokubaliana kwenye mkutano huu”. Alisistiza Mkuya.
Mikutano hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. Hali ya hewa ni baridi kiasi.
Imetolewa na Msemaji :Wizara ya fedha
Ingiahedi C.Mduma
Washington DC
16/04/2015
Ingiahedi C.Mduma
Washington DC
16/04/2015
Post a Comment