Mkurugenzi
wa JITENG Consultant Company Bw. Andrew Huwang akiongea jumuiya ya
wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania kuhusu ushiriki wao katika
masuala ya ukusanyaji kodi na kuendelea kuongeza ushirikiano kwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Semina
iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na
sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni
Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania(TRA) Bw.Yeremiah Mbaghi.
Afisa
Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bi. Rose Mahendeka akiongea na jumuiya ya wafanyabiashara
kutoka China waishio Tanzania kuhusu faida za Mfumo mpya wa Uondoshaji
Mizigo (TANCIS) unaosaidia kuongeza ufanisi katika uondoshaji wa Mizigo
ya wateja na kuondoa malamiko ya ucheleweshwaji wa huduma hiyo pia
kuondoa tatizo la upotevu na mizigo pindi inapoingizwa nchini, wakati wa
Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio Tanzania na Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha kuhusu ukusanyaji na
sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja akiwaeleza wafanyabiashara kutoka
China waishio Tanzania kuhusu umuhimu wa kushiriki katika matumizi ya
Mashine za Risiti za Kielektroniki (EFD) katika manunuzi na uuzaji wa
Bidhaa mbalimbali ili kuiwezesha serikali kupata mapato stahiki bila
udanganyifu wakati wa Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya wachina waishio
Tanzania na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaeleimisha
kuhusu ukusanyaji na sheria mbalimbali za Kodi Nchini leo Jijini Dar es
Salaam.
Wanajumuiya
wafanyabiashara kutoka China waishio Tanzania wakimsikiliza Afisa
Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja wakati wa Semina iliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.(Picha na HASSAN SILAYO-MAELEZO).
Post a Comment