Hashim Mbita azikwa leo makaburi ya Kisutu

Viongozi mbali mbali wa Dini ya Kiislam wakishiriki pamoja na waumini wao kwenye Ibada ya kuuswalia mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na baadae kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo.
Maelfu ya waunini wa kiislam wakishiriki kuubeba mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita wakati wakiutoa kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na tayari kwa kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiongoza shughuli ya kuusafirisha mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kuelekea kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo

Post a Comment

Previous Post Next Post