- Wakazi wa eneo Hili walalamika kuwa sasa ni zaidi ya Miezi minne hakuna hata dalili za kuijenga Barabara hii
- Sasa eneo hili limekuwa Pori rasmi ambapo hakuna hata pakupitisha Bajaji , Pikipiki na Hata Baiskeri kukatiza kwa shida
- Mmoja wa kiongozi wa Serikali za mtaa huu anaishi njia hii hii lakini sasa hatujui kama anaina haya au lah
- Huu ni Mtaa wa Maendeleo ambapo Kuna kituo kikubwa cha Afya cha Kiwanja Mpaka sasa hivi kweli hapa inakuwaje?
- Ungana nasi kushuhudia msije mkazania tunawaonea....
Huu
ni mtaa wa mpaka uliopo Sokomatola ambapo kwa kuangalia tuu hapa katika
kibao utagundua kuwa ni eneo ambalo limesha sahaulika kitambo sana.
Tazama
hiki kifusi kwa makini sana utagundua ni kweli kipo hapa kwa zaidi ya
miezi minne lakini wanakiangalia tuu, au zamu yao mpaka sasa haijafika?
Cha
kusikitisha zaidi tazama hiki kifusi ambapo njia hii ndiyo ingeweza
ikawa inafikika kwa haraka zaidi katika kituo cha afya kikubwa kabisa
cha Kiwanja mpaka , sasa hapa Gari zinapitaje? Msomaji wetu na wewe
Jiulize.
Hapa
picha halisi inaonesha wazi kuwa Kifusi hiki kimeanzia barabarani
kabisa kwenda chini Njia nzima imezibwa sasa je hii ni haki au
Mkandarasi wa Jiji anaweza kuwa na majibu hapa kwa nini mpaka sasa
ukarabati huu haujafanyika.
Ukiangalia kwa umakini kabisa utaona kuwa hapa ni ishara tosha inayotutambulisha kuwa eneo hili kuna kiongozi anapatikana.
Sasa
Mwenye macho haambiwi tazama Wote mtatusaidia kweli hii ni sawa? Je
Diwani wa kata hii ya Maendeleo upo? na Pia wananchi au wakazi wa mtaa
huu mmewasikia kiliochao? Na vipi kuhusu Jiji Mkandarasi unaonaje hii?
Ni
kweli tumeona mmeonesha moyo mmeweka kifusi ... hatuna pingamizi lakini
sasa kifusi kinaishi zaidi ya miezi minne tena au ndio kihifadhio eneo
hili?
Basi sawa hii Sintofahamu Tunawaachia wasomaji wetu, Tunakaribisha maoni yenu juu ya hili.
Kumbuka Tochi ya Mbeya yetu inaendelea kumulikia Jiji kona zote.. Endelea fuatilia... Maendeleo ni Muhimu Jiji liwe jiji Kweli.
Na Mbeya yetu.
Post a Comment