Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Richard Mwilipanga Lupembe (mstaafu) kilichotokea tarehe 30 Machi 2015,
Brigedia Jenerali Lupembe (mstaafu) alizaliwa mwaka 1945 katika Wilaya ya Njombe, Mkoa wa Njombe, Kijiji chaUtengule, Kata ya Lupembe, Tarafa ya Lupembe.
Alisoma shule ya Msingi Malangali, Shule ya Sekondari Malangali na shule ya Sekondari H.H. Agakhan na kuhitimu Kidato cha Sita mwaka 1964.
BrigediaJenerali Lupembe alijiunga na Jeshi tarehe 26 Agosti, 1964 na Kutunukiwa kamisheni tarehe 28 Julai, 1966. Alistaafu utumishi Jeshini kwa umri tarehe 30 Juni, 1998.
Katika utumishi wake alishika madaraka mbalimbali ikiwemo Mkurugenzi wa Utendaji Kivita Makao Makuu ya Jeshi, Mkuu wa mafunzo, na Mwambata Jeshi, Msumbiji, 1993hadi alipostaafu utumishi Jeshini tarehe 30 Juni 1998.
Marehemu ameacha mke na watoto.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 04 Aprili, 2015 kuanzia saa 3:00 hadi 4:00 asubuhi katika eneo maalumu la hospitali kuu ya Jeshi Lugalo na baadaye kupelekwa nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kuagwa kifamilia kisha mazishi rasmi kufanyika saa 9:00 Alasiri katika makaburi ya Kinondoni.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI RICHARD MWILIPANGA LUPEMBE (MSTAAFU) AMINA
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na MahusianoMakao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 -309963
Post a Comment