JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
VIDOKEZO
VYA HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. MATHIAS CHIKAWE
ALIPOZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO 14 APRILI 2015 JIJINI DAR ES SALAAM
KUHUSU MUSTAKABALI WA NCHI KUELEKEA ZOEZI LA KURA YA MAONI YA KATIBA
INAYOPENDEKEZWA NA UCHAGUZI MKUU UJAO
Kwamba Tanzania inaelekea
katika matukio makubwa muhimu ya Upigaji Kura ya Maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa
na Uchaguzi Mkuu.
Uzoefu unaonyesha kuwa wakati
kama huu, matukio ya kuashiria uvunjifu wa utulivu na usalama nchini hutokea.
Huko Visiwani Zanzibar,
tayari zimetolewa taarifa kuhusu matukio ya uchomaji wa baadhi ya Ofisi ya
Vyama vya Kisiasa na kuna taarifa za kuvamiwa wafuasi wa chama mojawapo ya
vyama vya kisiasa Visiwani humo wakati wakitokea katika mkutano wa chama chao.
Aidha kuna dalili za baadhi
ya Vyama vya Kijamii na Taasisi za Dini kuacha shughuli zao za kikatiba na
kuingilia masuala ya kisiasa, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria iliyosajili
Vyama na Taasisi hizo.
Wananchi na Viongozi
wanashauriwa kutekeleza majukumu yao ya kijamii na kisiasa kwa uhuru bila
kushawishi au kushawishiwa na kikundi au mtu yeyote.
Serikali inatoa tahadhari
kwa mtu yeyote, kikundi, Chama cha Kijamii, Taasisi ya Dini, au Chama cha
Kisiasa kitakachokiuka sheria za utendaji wa shughuli zake na kuhatarisha amani
na usalama wa raia na mali zao kuwa kitachukuliwa hatua za kisheria.
Ushauri umetolewa pia kwa
Vyama vya Siasa kuepuka kuanzisha misafara wakati wa kuandaa mikutano yake ili
kuepuka migongano baina ya wanachama wa vyama hasimu na pia kuwapunguzia askari
mzigo wa shughuli za ulinzi.
Kwa upande mwingine,
Serikali imechukua tahadhari zote kuhusu matishio ya vitendo vya ugaidi na
itashirikiana na Serikali ya Kenya kuhusiana na Watanzania wawili waliokamatwa
nchini Kenya kwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi.
Kwamba Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi ina taarifa za wageni wote walioingia nchini kihalali na kwa njia
nyinginezo na kwamba zoezi la kuwabaini raia wa kigeni wanaoingia nchini
kinyemela linaendelea.
Kwamba kuanzia tarehe 20
Aprili, 2015 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itaanza zoezi la kuvifuta katika
Daftari la Msajili
Vyama vyote vya Kijamii na
Taasisi za Dini zilizosajiliwa chini ya Sheria ya Vyama, Sura 337 ambavyo
haviwasilishi Taarifa zao za mwaka za ukaguzi wa hesabu na kulipa ada za mwaka
kama sheria inavyotaka. Zoezi hili
litaanza na Mkoa wa Dar es Salaam na litaendelea nchi nzima. Majina ya Vyama na Taasisi zitakazofutwa
yatawekwa katika Tovuti ya Wizara na
havitaruhusiwa kuendelea na shughuli zake.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
14
APRILI, 2015
إرسال تعليق