Mashua ya wahamiaji iliyozama
Umoja
wa Mataifa unasema unahofia kuwa huenda watu 800 walifariki siku ya
Jumapili, pale mashua waliyokuwa wakilitumia kuvuka bahari ya
Mediterenean ilipozama karibu na Libya.
Shirika la Umoja wa
mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR, limekuwa likizungumza na
manusura baada ya kuwasili katika kisiwa cha Sicily mapema leo Jumanne.

Mkuu wa sera kwenye Muungano wa
Ulaya Federica Mogherini anasema kuwa pana haja ya kuwepo hatua za
haraka ili kushughulikia suala kuhusu wahamiaji katika bahari ya
Mediterranean, huku akizindua mikakati kumi ya mpango wa kutanzua vifo
vya wahamiaji.
Mogherini, anasema kuwa mipango hiyo ni hatua kubwa
ya kuzuia kupotea kwa maisha ya watu. Majukumu ya muungano huo ni
kuzidisha operesheni ya uokozi, pamoja na mipango mipya ya kuharibu
mashua zinazotumiwa na walanguzi wa binadamu wanaowavusha watu baharini.
إرسال تعليق