SEGEREA,
DAR ES SALAAM
MAKONGORO MAHANGA
Segerea ni moja kati ya majimbo nane ya uchaguzi jijini Dar es Salaam. Katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi, Segerea ilikuwa ndani ya Jimbo la Ukonga ambapo Dk. Makongoro Mahanga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), alikuwa mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 2000 hadi 2010 lilipogawanywa na kuwa majimbo mawili ya Ukonga na Segerea.
Katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Dk. Mahanga alihamia Jimbo la Segerea alikoshinda kwa mbinde baada ya kupata ushindi wa asilimia 41.7 akiponea chupuchupu kuangushwa na Fredy Mpendazoe aliyepata asilimia 37.49 kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akifuatiwa na Kimangale Musa aliyepata asilimia 17.94 kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF.
Changamoto kubwa alizonazo Dk. Mahanga kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ni kwamba bado wananchi wake wanalalamikia kero mbalimbali zinazowasumbua, ikiwemo uhaba mkubwa wa maji na miundombinu mibovu, zikiwemo barabara na huduma shuleni.
Tayari Julius Mtatiro kupitia CUF, ametangaza kugombea kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ingawa jimbo hilo ni miongoni mwa majimbo kadhaa ambayo wagombea wa Ukawa wamegongana lakini duru za kisiasa, zinaonesha uwezekano mkubwa ni kwamba Mtatiro ataachwa agombee.
Mtatiro, kijana msomi mwenye shahada ya uzamili katika sanaa (Masters Degree in Arts), pia anaendelea kusomea shahada ya sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ni mkazi wa jimbo hilo kwa zaidi ya miaka 12, anatajwa kuwa na ushawishi mkubwa jimboni humo, hasa kama atapata sapoti kutoka kwa vyama vingine vinavyounda Ukawa.
“Mwaka 2010, Dk.Mahanga alishinda kimagumashi, sasa mwaka huu Ukawa wameungana hivyo kuna uwezekano wa kumuangusha, matokeo ya serikali za mitaa yametoa majibu kwamba Ukawa walishinda mitaa mingi kuliko CCM,” alisema Ibrahim Shekifu, mkazi wa jimbo hilo.
Endapo upepo wa kisiasa ukiendelea kuvuma kama hali ilivyo sasa, uwezekano wa Mheshimiwa Mahanga kushinda ni mdogo huku Ukawa wakitabiriwa kushinda kama walivyofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa

إرسال تعليق