IMEVUJA! Baada ya uhusiano wake na Mbongo Fleva, Malick Bandawe
kuvunjika, staa wa sinema Bongo, Rose Ndauka kwa sasa anadaiwa kuzama
kwenye penzi zito la Prodyuza wa Bongo Fleva, Emmanuel Saimon Sewando
‘Manecky’.
Msanii nyota wa sinema za Bongo Movie, Rose Ndauka.
Kwa mujibu wa chanzo, kwa muda mrefu wawili hao wamekuwa wakionekana
sambamba kama kumbikumbi hasa nyakati za usiku katika maeneo tofauti
ikiwemo studio ambayo Manecky anafanyia kazi zake na sehemu nyingine.
“Rose na Manecky ni wapenzi kwani muda mwingi wako pamoja, wanaongozana
kama kumbikumbi hasa usiku. Huwa tunawaona wanakuja maeneo ya hapa
Afrika Sana wanakwenda kununua chakula cha jioni huku Manecky akijinadi
kuwa ameamua kuwa na Rose kwa kuwa mke wake halali hivi sasa ni
mjamzito,” kilisema chanzo hicho.
Prodyuza wa Bongo Fleva, Emmanuel Saimon Sewando ‘Manecky’.
Mara baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu aliwatafuta wawili
hao ili kuweza kujibu tuhuma hizo ambapo Manecky alipopatikana
alikanusha na kudai ukaribu wao unaletwa na kazi. “Ukaribu wangu mimi na
Rose ni kazi tu kwani kuna ‘project’ tunaifanya nadhani mwenyewe Rose
ndiyo anaweza kuweka wazi hilo, kingine Rose anafanya kazi na mdogo
wangu kwenye gazeti la Rozzie la mtandaoni,” alisema Manecky.
Alipoulizwa kama ameamua kutembea na Rose kwa sababu mkewe ni
mjamzito, Manecky alizidi kusisitiza kuwa si kweli. “Hamna kitu kama
hicho jamani.” Ili kupata upande wa pili, mwanahabari wetu alimvutia
waya Rose ili kujua anazungumziaje tuhuma hizo likiwemo suala la
kuonekana na Manecky mara kwa mara, naye aliruka viunzi:
“Hakuna kitu kama hicho jamani, kwani mimi nachaguliwa mtu wa kukaa
naye? Acheni kusikiliza maneneo ya watu halafu Manecky ana mke ambaye ni
mjamzito na anatarajia kujifungua muda wowote,” alisema Rose. Rose na
Malick kabla ya kumwagana miezi michache iliyopita, walidumu kwenye
uhusiano kwa miaka kadhaa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja
إرسال تعليق