Rais
wa Afrika kusini Jacob Zuma ameahirisha ziara yake ya ughaibuni
kutokana na hali ya ghasia za kibaguzi dhidi ya wageni katika taifa
lake.
Alitarajiwa kuhudhuria mkutano nchini Indonesia.
Polisi
nchini Afrika Kusini wamewaagiza raia kutotuma ujumbe usiothibitishwa
kuhusu mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni kwa sababu hatua hiyo inazua
hofu.
Polisi wanesema kuwa kuna wasiwasi kuwa uvumi huo unachochea ghasia dhdi ya wahamiaji.
Watu 30 waliakamatwa wakati wa ghasia za usiku kucha mjini Johannesburg.
Biashara kadha zinazomilikiwa na raia wa kigeni ziliharibiwa.
Takriban
watu watano wameuawa kwenye mashambulizi yaliyaonza baada mfalme wa
kizulu Goodwill Zwelethini kusema kuwa wageni wanahitajka kuondoka
Afrika Kusini
Post a Comment